Google Visitor Experience
Kazi za sanaa
za nje
Tunakualika ugundue kazi za sanaa katika uwanda wa nje kwa kugusa, kudadisi na kucheza. Zikihamasishwa na Mradi wa Burning Man, kazi sita shirikishi na bunifu za sanaa zilichaguliwa kwa ushirikiano na jamii ya eneo la Mountain View. Katika mfululizo wa mikutano iliyohamasisha mitindo ya kazi za sanaa, tulisikiliza simulizi za utotoni za jamii kuhusu matukio ya udadisi na ya kusisimua, tukajifunza jinsi watu hupata mwelekeo kupitia matukio muhimu na tukatamani sana matukio ya ucheshi. Tunatumai kuwa nafasi hii mpya ya sanaa ya nje itaboresha miunganisho ya kawaida na kuunda uhusiano wa kibinadamu kupitia sanaa shirikishi na nyumbufu.
Mkusanyiko wa sanaa
ya ndani
Mpango wa Google wa "Artist in Residence" hutambua wasanii kama wavumbuzi muhimu wanaohamasisha ubunifu katika jamii tunakoishi na kufanya kazi. Tunawapa wasanii kazi ya kutayarisha kazi halisi za sanaa katika maeneo ya Google duniani kote na kazi yao ya sanaa katika maeneo kama vile Google Visitor Experience hukuza malengo ya mpango ya kuendeleza jamii, kuhamasisha ubunifu, na kukuza uvumbuzi. Katika Google Visitor Experience, unaweza kupata kazi ya sanaa ya "Artist in Residence" kwenye Cafe, Huddle na Google Store. Wasanii ni pamoja na Kelly Ording, John Patrick Thomas, Miguel Arzabe, na Angelica Trimble-Yanu, wanaoishi eneo la Bay Area.