Tunajitahidi kuunda nafasi za kazi zenye ufanisi na ambazo zinafurahisha. Ni kipimo chetu cha tatu kinachotusaidia kujihisi tumeshirikishwa, tumechangamshwa na kuridhika kwa kutukumbusha kuhusu ubinadamu wetu wa pamoja. Sanaa ni njia ya kushirikisha ya kutumia ubinadamu huu na tangu mwaka 2010 tumeanzisha mipango kadhaa ya sanaa katika Google, ikiwemo Mpango wetu wa ndani wa GoogleArts, mpango wa Sanaa na Utamaduni kwenye Google pamoja na mpango wa Google wa "Artist in Residence".
Katika Google Visitor Experience (iliyo katika ofisi mpya ya Gradient Canopy ya Google), mpango maalum wa sanaa ya umma unaeneza mtazamo huu kwa jamii yetu pana ya Mountain View. Kazi sita za sanaa ya umma zilizotandazwa katika uwanda wa nje wa umma na katika njia za kutembelea zinasaidia kufanya Google Visitor Experience kuwa mahali pa kusisimua kwa kila mtu.
Zikiwa zimetayarishwa na wasanii wa karibu na wa mbali, kila mojawapo ya kazi hizi za sanaa iliundwa mahususi kwa sehemu ilipo, ikisaidia kuanzisha sehemu za kukusanyika karibu na jengo na kuleta fursa za kucheza na za kufurahisha. Wakati huo huo, kazi za sanaa huendelea na malengo ya utunzaji wa mazingira na nyenzo bora ya Gradient Canopy, kwani kila kazi ya sanaa imeundwa kutokana nyenzo ambazo Hazijaorodheshwa kwenye orodha ya Red List (kumaanisha kuwa zinaepuka viungo ambavyo ni hatari sana kwa afya ya binadamu na mazingira) na zinasaidia juhudi za kutokuwa na taka. Kama tu nyenzo zilizo ndani na zilizo kwenye jengo, kazi za sanaa zinachangia juhudi za Gradient Canopy kupata cheti cha Kiwango cha Nyenzo kwenye Living Building Challenge (LBC) kutoka taasisi ya International Living Future Institute (ILFI).
Tulipokuwa tukibuni sanaa za umma katika Gradient Canopy, lengo letu lilikuwa kubaini sanaa zinazoshirikisha na kusisimua ambazo zingefanya uwanda wa nje kuwa sehemu ya ugunduzi na ambayo unatamani kurudi tena. Kwa kifupi, hamu ilikuwa ya sanaa ambayo haifai sana kwa jumba la makumbusho, bali iwe kama sanaa zinazoshuhudiwa katika tukio la Burning Man katika Jiji la Black Rock, ambalo ni jiji la muda la kila mwaka katika jangwa la Nevada maarufu kwa kazi za sanaa za sehemu mahususi zinazoibua hisia. Tukitafuta mshirika wa kuhakikisha kuwa sanaa ya uwanda wa nje inapatikana, tulifanya kazi na shirika lisilolenga faida la Mradi wa Burning Man, ili kudhibiti mchakato wa kuchagua sanaa unaoongozwa na jamii. Kutokana na kujitolea kwao kikamilifu katika kushirikisha jamii, Mradi wa Burning Man ulilingana na lengo letu la kuunda sanaa ya umma itakayoshirikisha na itakayoleta hisia ya pamoja ya ubunifu.