Kupitia Bay View na Gradient Canopy, tulitaka kukuza maeneo mazuri na ya kuvutia yanayoongoza katika kuhakikisha miundo endelevu na yenye manufaa kwa jamii na Google. Vyovyote vile, tunajitahidi kila wakati kuwa jirani mwema. Kwa sababu hiyo, katika Gradient Canopy tuliangazia kukuza nafasi za jamii zinazojumuisha kila mtu na kuvutia majirani, wageni na WanaGoogle. Kwetu sisi, kando na kubuni maeneo bora zaidi ya kufanyia kazi, tunajitahidi pia kuweka njia mpya za mahusiano zinazosaidia jamii zetu za karibu kustawi.
Kuunda sehemu
Designing vibrant places that respond to their local context and create benefits for everyone.
Dakika 3
Mchoro wa awali unaoonyesha eneo la umma katika Gradient Canopy.
"Tunauliza jinsi maeneo haya yanaweza kuwa na manufaa ya kimazingira na ya kijamii kwa kila mtu yanayohusisha,"
– Joe Van Belleghem, mkurugenzi mkuu wa Google wa maendeleo ya dunia
Katika Gradient Canopy, tulimakinika kuhakikisha kuwa jengo linaendana vizuri na mazingira. Mzingo maalum wa Kijani wenye njia za baiskeli na wanaotembea kwa miguu unazunguka jengo na kupita kwenye eneo hilo la eka 18. Hapa watu wanaweza kufurahia mandhari asili na sanaa ya umma iliyo kwenye sehemu za nje ya jengo zinazotumika na umma.
Upande wa magharibi, jengo liko mkabala na Charleston Park, hali inayokaribisha umma kwenye Google Visitor Experience. Iwe unatangamana na marafiki kwenye Cafe, kuhudhuria tukio kwenye Huddle, kuangalia bidhaa na huduma kwenye Google Store, kugundua biashara za karibu katika Duka la Muda au unadadisi kuhusu sanaa na usanidi katika Plaza, kuna kitu kwa kila mtu. Huddle inatoa matukio na warsha mbalimbali ili kuangazia mashirika ya karibu ya jamii na yasiyolenga faida, huku ikitumika kama kituo cha kijamii cha tawi la Mountain View na eneo pana la North Bayshore.
Sehemu hizi za ndani za jamii huungana na kuwa uwanda mkubwa wa nje wa umma, ambapo tutaandaa matukio ya maeneo jirani na kukuza mahusiano muhimu miongoni mwa jamii na WanaGoogle. Pia, kuna vipande sita vya sanaa ya umma kote kwenye plaza na viti vya kutosha vya umma.
Soko la Wakulima la Mountain View kunakoendelea shughuli nyingi.
Ili kuboresha jinsi watu wanavyosafiri katika eneo la North Bayshore, tumeshirikiana na Jiji la Mountain View kujenga awamu ya kwanza ya Ukanda wa Usafiri wa Umma wa Charleston, ambao utahimiza usafiri wa umma, kuongeza usalama kwa wanaotumia baiskeli na wanaotembea kwa miguu na kufanya iwe rahisi kusafiri katika eneo la North Bayshore bila gari. Kama sehemu ya mradi wa Gradient Canopy, vituo viwili vya usafiri wa umma vilijengwa kwenye Barabara ya Charleston, karibu na tawi. Vituo hivi, pamoja na njia zilizopangwa za mabasi pekee kwenye Barabara ya Charleston na Shoreline Boulevard, vitaboresha chaguo za usafiri wa umma katika eneo hilo.
Ukanda wa Usafiri wa Umma wa Charleston pia unaangazia njia za kiwango cha kimataifa za baiskeli na wanaotembea kwa miguu – ikiwa ni pamoja na njia za baiskeli za Daraja la IV, zinazojulikana pia kama njia za wanaoendesha baiskeli. Ndani ya jengo, tunahimiza usafiri kwa kutumia “magurudumu mawili” kwa kuweka nafasi zaidi ya 780 za maegesho ya baiskeli, pamoja na makabati ya kufungia baiskeli na mabafu ya manyunyu.
Ujumbe kwa wasomaji: Hadithi hii ilichapishwa Mei 2022 na kusasishwa Agosti 2023 ili kujumuisha maelezo ya mradi ya hivi majuzi zaidi.