Katika Gradient Canopy, ambako tumefanikiwa kupata cheti cha Kiwango cha Nyenzo kwenye Living Building Challenge (LBC) kutoka taasisi ya International Living Future Institute (ILFI), kutafuta njia za kujumuisha nyenzo zisizo na sumu na zinazorejesha mfumo ikolojia ilikuwa muhimu sana. Kwa sababu hii, tumegundua njia za kujumuisha mbao zilizobanwa pamoja zinazopatikana kwa njia endelevu katika jengo ili kunufaika na sifa za mbao za utwaaji wa hewa ya ukaa.
Mbao zilizobanwa pamoja ni mbinu ya ujenzi inayotumia mbao zilizobanwa pamoja ili kuunda nguzo, mihimili, kuta, sakafu na paa kwa njia inayoweza kupunguza kaboni iliyojumuishwa ikilinganishwa na mbinu za kiasili za ujenzi. Hatimaye, mbao zilizobanwa pamoja zimetumika sana katika jengo hili na tulichojifunza hapa tumezingatia kwenye miradi mingine ya ujenzi katika Google.
Tumevutiwa kwa muda na uwezo wa mbao zilizobanwa pamoja kwa sababu zinakuza sehemu za kazi zenye afya, tija zaidi na zenye mwonekano unaovutia kupitia sifa zake za kuunganisha watu na mazingira asili. Ashiki ya biolojia inahusu kuunganisha mazingira na mipango ya kuunda nafasi ambako watu wanaweza kustawi. Kujumuisha nyenzo za mbao zisizo na rangi kwenye jengo hakupunguzi tu hitaji la kutumia nyenzo za ziada kama vile mipako na rangi, lakini pia husaidia watu wajihisi kuunganishwa na mazingira hata wakiwa ndani ya jengo. Kwa hivyo, tulipoanzisha muundo wa Gradient Canopy, tulizingatia hapo awali uwezekano wa jengo lote kuwa la mbao zilizobanwa pamoja na tukabaini kuwa majengo haya hayangedumu kwa muda mrefu jinsi tungependa, hata hivyo bado tumeweza kujumuisha mbao katika baadhi ya sehemu za miundo ndani ya jengo.
Katika Gradient Canopy, nyenzo za mbao zilizobanwa pamoja zimechukua umbo la sehemu ya mbao zilizounganishwa kwa kuvuka (CLT), muundo wa mbao zilizoundwa kwa kuunganisha safu nyingi za mbao zilizopasuliwa ili kufikia uthabiti bora wa muundo. Tulianza kutumia CLT kama mbao za ujenzi (sehemu ambako saruji humwagwa) kwenye kiwango cha pili cha sakafu ya saruji, ambako zinaimarisha kwa njia mbalimbali. Tumezitumia kwa njia ambayo badala ya kuondolewa na kutupwa kama ilivyo kawaida baada ya saruji kukauka, CLT huachwa hapo ili zitumike kama dari ya mbao zisizo na rangi katika sehemu za ghorofa ya chini na reli za usalama zinazozunguka uga wa ndani. Pia mbao hutumika kwenye milango na fremu za milango katika jengo nzima, hususan kwa podi na vyumba vya mkutano. Kwa haya, timu iliweza kufanya kazi pamoja na mtoa huduma na kupata cheti cha lebo ya Declare kwa mkusanyiko mzima wa mlango, hivyo kutusaidia kupea kipaumbele nyenzo za ujenzi zinazoonyesha kemia salama ili kuunda mazingira mazuri ya ndani.