Tangu kuanzishwa kwa Google, tumekuwa tukiamini kwa dhati kwamba mafanikio ya kampuni yetu yanatokana na juhudi za wafanyakazi wetu. Ndio maana tumekuwa tukilenga kubuni maeneo yetu tukizingatia furaha na ustawi wa jumla ya WanaGoogle. Hapa Gradient Canopy, mtazamo huu wa kumzingatia mtumiaji kwanza unaangazia hadi moja ya mawazo makuu ya muundo tuliyotumia kupanga eneo la ndani: kugawanya jengo katika ghorofa mbili pekee. Hapa, maeneo ya kazi na vyumba vya timu viko kwenye ghorofa ya juu vikiwa na “nyuga” nyingi zinazoziunganisha na sehemu za huduma kwenye ghorofa ya chini iliyo na vyumba vya mikutano, nyuga na vyumba vyote vya timu.
Nafasi za kazi kwenye ghorofa ya pili ziliundwa kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira, ubadilikaji na kwa madhumuni ya kazi. Ghorofa yote ya juu ina vyumba, kuta na samani za magurudumu zilizoundwa mapema. Hali hii huruhusu unyumbufu, ambapo vyumba vinaweza kubadilishwa kwa urahisi bila taka yoyote kwani vifaa vile vile vinaweza kutumika tena katika mipangilio mipya. Ghorofa hii pia ina sehemu kubwa inayofaa kazi, wakati ghorofa ya chini ina vyumba vya kushirikiana mahususi kwa mapumziko ya mwili na akili siku nzima.
Nyuga za ndani za ghorofa ya kwanza ya Gradient Canopy zinaziwezesha timu zetu kwa kusaidia kuwaleta watu pamoja na kuhakikisha kuwa kila mtu anapata mazingira bora yanayochochea tija. Katika ofisi za kawaida, unaweza ukaona vipengee mbalimbali vya mipango na sehemu za huduma pamoja na vyumba vya maeneo ya kazi. Jumla ya nyuga 20 zenye ngazi zinazoounganisha ghorofa mbili, hali inayorahisisha kufikia huduma pamoja na kutumika kama sehemu za matumizi mbalimbali ambako timu zinaweza kutumia kama sehemu nyumbufu inayoweza kutumika kwa shughuli mbalimbali.
Kando na kusaidia kutenganisha sehemu za kumakinika na zenye shughuli nyingi ili watu waweze kufanya kazi bora, nyuga pia zinatoa manufaa ya kibayolojia na husaidia WanaGoogle kupumzika wakati wa mchana. Tunafahamu kuwa miundo bora zaidi inaonyesha uhusiano wa kina kati ya mazingira na afya ya binadamu, hivyo tumejumuisha kanuni za muundo wa kibiolojia katika Gradient Canopy ili kuunda mahali ambako watu watafanikiwa. Miundo ya kibayolojia ina aina mbalimbali za maeneo yanayohimiza msisimko wa hisia nyingi, hali sawa na ambayo mtu anapata katika mazingira asili. Nyuga husaidia kuhimiza manufaa ya kifiziolojia ya shughuli za kimwili wanapozunguka kati ya ghorofa mbili, hali inayowapa watu njia mpya za kufika katika maeneo mbalimbali katika jengo ambazo zinaweza kusisimua akili zao na kuhamasisha ubunifu siku nzima. Pia zinasaidia kupenyeza mwanga wa asili katika ghorofa ya chini kupitia kwenye madirisha ya juu, hali inayosaidia utendaji bora wa mfumo wa mabadiliko ya mwili katika kipindi cha saa 24.