Kwa miongo kadhaa, tumetafuta jinsi ya kubuni mazingira bora zaidi ya ndani. Iwe ni hadithi za waanzilishi wa Google wakitembea katika majengo yetu ya awali wakipima ubora wa hewa ya ndani kwa kutumia vihesabio vishikizi vya chembe au kukagua maelfu ya bidhaa kwa miaka mingi ili kuhakikisha kuwa hatuleti sumu kwenye sehemu zetu za ndani zilizoboreshwa, tumekuwa na lengo la muda mrefu la kuunda nafasi bora za kazi. Tuna fahari kuwa Gradient Canopy ni mojawapo ya miradi mikubwa zaidi uliopata cheti cha Kiwango cha Nyenzo kwenye Living Building Challenge (LBC) kutoka taasisi ya International Living Future Institute (ILFI), inayolenga kusaidia kuunda uchumi wa nyenzo zisizo na sumu, unaorejesha mazingira na uwazi.
Tulizipa kipaumbele nyenzo ambazo ni bora kwa watu pamoja na mazingira katika Gradient Canopy na Google Visitor Experience. Kila nyenzo iliyowekwa kwenye jengo imekaguliwa na mtengenezaji ili kuhakikisha kuwa haina viungo vilivyoorodheshwa kwenye orodha ya 'Red List' ya LBC, vinavyowakilisha kemikali hatari zaidi ambazo huathiri afya ya binadamu na mazingira. Kwa jumla, zaidi ya bidhaa 8,000 zilikaguliwa katika Gradient Canopy, tukifanya kazi pamoja na watengenezaji wanaoshiriki katika juhudi zetu za kuhimiza uwazi katika sekta ya ujenzi.
Mtazamo wetu wa nyenzo bora katika Gradient Canopy huenea mbali zaidi kupita sehemu za ndani na WanaGoogle wanaofanya kazi humo kila siku. Kwa kuangalia nyenzo za ndani na za nje ya jengo, ikiwa ni pamoja na kazi sita za sanaa ya umma zilizowekwa nje ya jengo, tunaipa kipaumbele afya ya jamii kwenye mfumo wa usambazaji pamoja na hatua anuwai za maisha kamili ya bidhaa zetu za ujenzi. Hii inamaanisha kuwa nyenzo, iwe ni vitu unavyoona na kugusa kama vile zulia na kuta au vile ambavyo havionekani kwa urahisi, kama vile mipako ya dirisha na kuhami ya jengo, zilikaguliwa kwa makini na watengenezaji husika ili kuhakikisha kuwa afya ilikuwa sababu kuu ya kuziteua.