Kwa kawaida, gereji za maegesho haziwakilishi ubora wa usanifu wa majengo - zinatumika katika jamii ambayo, kwa wengi, bado inategemea magari kuwasafirisha watu wanakoenda. Lakini tunapotarajia mustakabali wenye magari machache na njia endelevu zaidi za usafirishaji zitakazosaidia kupunguza uzalishaji kaboni na msongamano wa magari, hitaji la nafasi za maegesho huenda likapungua. Kwa hivyo, gereji za maegesho zenye matumizi moja zinaweza kukosa umuhimu na kubomolewa hivyo basi kusababisha kuongezeka kwa taka, kaboni na gharama. Ndiyo maana Alta Garage mpya ya Google katika eneo la Mountain View iliundwa kimakusudi isiwe gereji ya kuegesha magari siku moja - na iko tayari kubadilishwa kwa matumizi ya kibiashara, makazi au jumuiya wakati wowote unaofaa.
Wazo hilo linarejelewa kama maegesho yanayoweza kutumika siku zijazo: Kadiri mahitaji ya jamii yanavyobadilika siku zijazo, ndivyo pia Alta Garage inaweza kubadilika. Je, unahitaji ofisi, nyumba, vistawishi au nafasi zaidi ya matukio? Alta Garage inaweza kubadilishwa iwe mojawapo ya hizo kadiri mahitaji ya maegesho yanavyopungua. Na inaweza kufanya hivyo kwa njia inayopunguza gharama, kuokoa muda, kupunguza taka na kuongeza uendelevu.