Kupitia Gradient Canopy, lengo mojawapo lilikuwa kujenga eneo la mradi kwa njia inayoendana na mandhari na kulifanya listahimili mabadiliko kadiri muda unavyosonga. Kwetu sisi, “kustahimili mabadiliko” kunamaanisha maeneo yanayochangia ubora wa kiikolojia wa muda mrefu wa eneo husika, ambapo watu na wanyamapori wanaweza kuimarika hata kukiwa na mabadiliko ya tabianchi. Katika Gradient Canopy, tulijitahidi kukuza upya vipengee vya kihistoria vya mfumo ikolojia vinavyotoa usaidizi muhimu kwa wanyamapori. Hata hivyo, tunaelewa kwamba kuna hatari kwa wanyamapori katika mazingira ya mjini, hususan kwa ndege wa eneo hili kama vile chiriku, jurawa, ndege wavumaji na ndege waimbaji. Kwa sababu hii, tulisanifu Gradient Canopy tukitumia mikakati kadhaa inayofaa ndege.
Vioo kwenye majengo vinaweza kuwa na athari kubwa kwa ndege, kwa hivyo ilikuwa muhimu kusanifu jengo, mandhari na mwangaza katika Gradient Canopy kwa njia inayoendana na Cheti cha LEED cha Uvumbuzi katika Usanifu: Kuzuia Mgongano wa Ndege ili kupunguza migongano ya ndege na jengo.
Ili kuelewa njia bora zaidi ya kujumuisha vipengee vya usanifu ambavyo ni salama kwa ndege, tulishirikiana na washauri wa ikolojia H.T. Harvey & Associates ili kufuata viwango na mapendekezo yanayoongoza ya kusanifu majengo salama kwa ndege. Hatimaye, tulijumuisha muundo unaofaa ndege kwa njia mbili kuu katika Gradient Canopy: kwanza kwa kupunguza uakisi na uwazi kwenye vioo vya jengo na pili kwa kupunguza uchafuzi wa mwangaza unaotokana na jengo wakati wa usiku kupitia mbinu za kuweka mwangaza ndani na nje
Vioo havionekani kwa ndege na binadamu, lakini binadamu hujifunza kutambua vioo kadiri muda unavyosonga kupitia ishara kama vile fremu za madirisha na uakisi. Kwa upande mwingine, ndege wana uwezo mdogo wa kutambua umbali wa vitu na mara nyingi wanatambua uakisi wa mandhari na anga kama kitu halisi. Uwazi kwenye vioo unaweza pia kusababisha migongano iwapo ndege anaweza kuona mimea kupitia kona za vioo au mimea iliyo ndani ya jengo. Kimsingi, kadiri uonekanaji wa mimea au anga ulivyo juu kupitia vioo vya jengo, iwe kutokana na uwazi au uakisi, ndivyo matukio ya migongano ya ndege yanavyoongezeka.
Katika Gradient Canopy, suluhu yetu ilikuwa kutafuta kwanza vioo vyenye kiwango cha chini cha uakisi. Maendeleo ya hivi majuzi katika teknolojia na utengenezaji wa vioo yamefanya iwe rahisi kupunguza kiwango cha uakisi wa nje bila kuathiri kiwango cha joto la jua kinachoingia kwenye jengo. Hali hii ilitusaidia kupata vioo bora vya madirisha na roshani nyingi za jengo. Kuweka alama zinazoonekana kwa karibu kwenye vioo, kama vile vibandiko au "michoro" ya kauri iliyopachikwa, kunaweza pia kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya ndege kwa sababu ndege wataona alama hizo kama kizuizi na hawatajaribu kuruka upande mwingine. Tulichagua muundo mzito wa alama kwa kufuata mwongozo wa sasa wa Hifadhi ya Ndege ya Marekani, unaolenga kutoa ulinzi zaidi kwa hata ndege wadogo zaidi. Katika Gradient Canopy, tulitengeneza michoro kwenye vioo vinavyoonekana kwa umma kama fumbo la maneno, ambapo majina ya aina 30 tofauti za ndege wa eneo hilo katika lugha 30 yamewekwa pamoja kwenye vioo. Ni “Kitu fiche” kinachoongeza hali ya kufurahisha na ugunduzi kwenye muundo wenye ufanisi sana ambao ni salama kwa ndege.