Je, unaweza kutueleza zaidi kuhusu upekee wa eneo hili?
Hali ya uvumbuzi katika eneo hili inahamasisha na huzungumziwa mara zote. Karibu kila mtu ana dhamira ya dhati ya kufanya mabadiliko duniani – hicho ndicho kinatutia motisha hapa Google na Alphabet pia ninaamini kuwa ndicho kinawatia motisha wengine wengi wanaoamua kuishi na kufanya kazi hapa. Kuna lengo katika eneo la Valley la kuunda mustakabali ambao tungependa kuona na ninafikiri kuwa ndilo linafanya eneo hili kuwa mojawapo ya maeneo maalum duniani.
Je, Google ina uhusiano upi na Mountain View?
Tangu 1999, Mountain View imekuwa makao ya Google na tunaona kuwa tutakuwa hapa kwa miaka mingi ijayo. Google ilichagua Mountain View kuwa makao yetu makuu kwa sababu tunapenda kila kitu kuhusu kuwa katika eneo hili. Tunapenda uzuri wa Bay, ukaribu na vyuo vikuu, mazingira yanayofaa familia pamoja na fursa ya kufanya kazi katika jiji lililo kwenye kiini cha Silicon Valley.
Wafanyakazi wetu wengi wanaishi na kufanya kazi katika Mountain View na kama kampuni, tunaamini kwa dhati katika kuwa jirani mwema. Katika miaka yote, tumewekeza mamilioni ya dola katika jamii, kwa kutoa ruzuku kwenye Taasisi ya Elimu ya Mountain View ili kufadhili elimu ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM), kufadhili Mountain View Community Shuttle, kutoa ruzuku ya kufadhili michakato ya kutatua ukosefu wa makazi na huduma za udhibiti pamoja na miradi ya kurejesha ikolojia kama vile Charleston Retention Basin, miongoni mwa miradi mingine.
Na tunajivunia kuwa kila mwaka, WanaGoogle hujitolea katika mashirika ya Mountain View kwa maelfu ya saa, ikijumuisha Shirika la Huduma za Jamii la Mountain View, Silicon Valley Bicycle Exchange, shule za Mountain View na Makumbusho ya kipekee ya Historia ya Kompyuta.
Je, Gradient Canopy na Bay View huendeleza vipi uhusiano wa muda mrefu wa Google na eneo hilo?
Gradient Canopy ni jengo letu la kwanza kabisa kujenga katika Mountain View na tulifikiria sana kuhusu njia bora ya kubuni mradi unaowakilisha maono ya Jiji hili kwa mustakabali wa North Bayshore. Gradient Canopy hutathimini upya mahali pa kazi kwa muundo wenye kusudio unaovutia jamii, kujumuisha mazingira asili ipasavyo, kubuni thamani kubwa ya kiuchumi kwenye jiji na pia kusaidia wafanyakazi wetu wanaopenda kuishi na kufanya kazi katika Mountain View.
Tangu kabla ya janga, sehemu ya umahiri wa nafasi zetu za kazi za Google ni kuwa nafasi hizi zinangatia afya, ni endelevu na zinaweza kutumika kwa shughuli mbalimbali, zikijumuisha “Ushirikiano”. Muundo mzuri hutengeneza mazingira ambayo watu wangependa kuwa, jambo linalodhihirishwa na karibu nusu ya wafanyakazi wetu wa kimataifa wanaokuja kwa hiari katika ofisi zetu mara tu zilipofunguliwa tena kwa usalama. Sasa, kupitia miradi yetu ya kujenga majengo kabisa, tunaweza kujumuisha wajibu huu pamoja na mafunzo mengi katika jamii ya eneo husika. Tumezingatia sana jinsi nafasi hizi zinaweza kushirikisha jamii na kukuza uthabiti na matokeo bora ya afya.